Monday, 31 August 2015

Tigo yazindua huduma mpya

Tigo yazindua huduma mpya Imeandikwa na Evance Ng’ingo Imechapishwa: 26 Agosti 2015 Mavumbuo: 375 Kuchapa Barua pepe Mkuu wa Huduma za fedha kwa njia ya simu wa Kampuni ya simu ya Tigo, Ruan Swanepoel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Chagua Tigopesa Inalipa’ ya kampuni hiyo, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga. (Picha na Fadhili Akida). 0 Comments KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, imezindua huduma mpya iitwayo Chagua Tigopesa inalipa, yenye lengo la kuwaongezea tija watumiaji wa huduma hiyo. Huduma hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel aliyeeleza kuwa mteja wa Tigo anayetumia Tigo pesa atapata riba kila baada ya miezi mitatu kulingana na kiasi cha fedha alichohifadhi katika simu yake. Alitaja huduma nyingine kuwa ni kifurushi cha bure kitakachotolewa kwa mteja atakayelipa huduma mbalimbali kwa kutumia Tigo pesa . “Kila mteja anapomnunulia mwenzake kifurushi, atajipatia asilimia 10 ya thamani ya kifurushi atakachokuwa amemnunulia mwenzake huyo,” alisema. Alitoa mfano kwa kusema, mteja wa Tigo akimnunulia mtu kifurushi cha Sh 10,000, atapata zawadi ya Sh 1000,” Swanepoel alisema. Alisema, tangu mwaka jana kampuni hiyo ilipozindua huduma ya kuwagawia salio wateja wake , imekwishatoa jumla ya Sh bilioni 27. Kwa maelezo yake, huduma hiyo inayotolewa kila baada ya miezi mitatu kwa mwisho wa mwezi Julai, mwaka huu, Tigo ilitoa jumla ya Sh bilioni 3.3 kwa wateja wake.

No comments:

Post a Comment